UTABIRI NI NINI?
Utabiri au ubashiri ni uoteaji au ukisiaji wa mambo yatakayotokea muda ujao.
Mtu mwenye uwezo wa kutabiri huitwa mtabiri.
Mara nyingine utabiri unatokana na uchunguzi wa kisayansi, kwa mfano utabiri wa hali ya hewa.
Katika dini mbalimbali utabiri unatokana na karama maalumu ambayo mtu anajaliwa na Mwenyezi Mungu.
MAANA YA MUDA KATIKA UTABIRI NINI?
Muda ni kipindi ambacho mtu aidha alifanya, anafanya au anatarajia kufanya jambo fulani. Katika maisha tumepitia vitu mbalimbali, baadhi tunaweza tukavikumbuka na vingine hatuvikumbuki, na katika maisha kadri muda unavyokwenda ndivyo vitu vinazidi kugunduliwa kutokana na ongezeko la sayansi.
Katika maisha ya kila siku mwanadamu hutegemea sana muda ili kufanikisha malengo yake.
Matumizi ya muda
Muda hutumika na watu mbalimbali kwa mambo mbalimbali kama itakavyoelezwa hapa chini:
mwanafunzi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujisomea.
mfanyakazi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.
Endapo watautumia muda huo vibaya, hakika hawataweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Hata hivyo ni muhimu kuwa na uwiano mzuri katika matumizi ya muda, kwa mfano, kwa sala na kazi
UTABIRI KATIAKA SAYANSI
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.
Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.
Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:
Sayansi Asili k.m.
Biolojia
Jiografia
Zoolojia
Sayansi Umbile k.m.
Fizikia
Hisabati
Kemia
Sayansi Jamii k.m.
Akiolojia
Elimu
Saikolojia
Siasa
Sayansi Tumizi k.m.
Teknolojia
Uhandisi
Pia, kuna sayansi zinazohusu mada mbalimbali:
Maarifa
Unajimu
Tiba
Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli za kisayansi.
Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.
Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.
Sura ya kisayansi
Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe (maada yabisi) kuna uvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu
0 Reviews:
Post a Comment