UTABIRI WA NDOTO
Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi.
Yaliyomo na malengo ya ndoto hayajaeleweka vizuri, ingawa tangu zamani yamejadiliwa sana katika sayansi (hasa elimunafsia) na katika dini. Fani inayochunguza ndoto kisayansi inaitwa onirolojia
Kwa kiasi kikubwa ndoto zinatokea wakati usingizini macho yanapogeukageuka zaidi, ambapo utendaji wa akili ni mkubwa karibu sawa na mtu anapokuwa macho. Zikitokea wakati mwingine wa usingizi, ndoto hazikumbukwi sana baada ya kuzinduka.
Muda wa ndoto unaweza kuwa tofauti sana: tangu sekunde chache hadi dakika 20–30.
Kwa wastani watu wanapata ndoto 3 hadi 5 kwa usiku, wengine hadi 7;lakini nyingi zinasahaulika mara au mapema.Watu wanaweza kukumbuka zaidi ndoto zao wakiamshwa wakati wa usingizi wa macho kugeukageuka.
Ndoto zinaelekea kudumu zaidi kadiri muda wa usiku unavyozidi kwenda.
Ndoto zinaweza kuwa za aina mbalimbali: nje za uwezekano katika maisha ya kawaida, za ajabuajabu, za kutisha, za kusisimua, za kishirikina, za kidini, za kusikitisha, za kijinsia, n.k. Zinaweza pia kumsaidia msanii kubuni kitu.
Kwa kawaida ziko nje ya udhibiti wa mtu, isipokuwa anapoota akiwa anajitambua (ndoto za mchana).
Rai kuhusu maana ya ndoto zimetofautiana sana kadiri ya nyakati na utamaduni
Kumbukumbu za zamani zaidi kuhusu ndoto ni za miaka 5000 hivi iliyopita huko Mesopotamia, ambapo zilichorwa katika vigae.
Katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale, watu walisadiki ndoto zinaleta ujumbe kutoka kwa mungu fulani au marehemu fulani na kwamba zinatabiri ya kesho.
Njozi
Jump to navigationJump to search
Njozi ni istilahi inayotumika hasa katika maisha ya kiroho kama njia ya mtu kupata taarifa ya mambo yaliyopita, yaliyopo, na yale yajayo.
Neno hilo hutumiwa pia kwa maana ya ndoto, ambayo ni ya kawaida pale mtu anapokuwa amepumzisha akili na mwili.
Upande wa dini huaminiwa kuwa Mungu hutumia njozi kuwasilisha ujumbe kwa mtu, kama habari juu ya kazi yake au tukio linalotaka kutukia. Kwa kifupi tu Njozi ni tukio lolote la ndoto inaweza kuwa nzuri au mbaya
0 Reviews:
Post a Comment