Jumapili
Jump to navigationJump to search
Jumapili ni siku ya kwanza katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya Kiyahudi-Kikristo. Iko kati ya siku za Jumamosi na Jumatatu.
Kwa Wakristo walio wengi ni siku ya sala za pamoja kanisani.
Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "2" ndani yake. Hili ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa, siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.
Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee, hasa kwa sababu Kiarabu, ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu, kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "al-ahad" yaani "ya kwanza".

Jumatatu
Jump to navigationJump to search
Jumatatu ni siku ya pili katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumapili na Jumanne.
Siku ya pili au siku ya kwanza?
Kuna nchi zilizobadilisha hesabu kufuatana na kawaida ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili ambako Jumatatu ni siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda rasmi za serikali hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia.
Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "3" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "ya pili".
Siku ya mwezi
Katika lugha mbalimbali za Ulaya siku hii ina jina la "mwezi". Lugha hizi kama Kiingereza, Kifaransa au Kijerumani zinaendeleza urithi wa Roma ya Kale na zaidi wa Babiloni ambako kila siku ya wiki ilikuwa chini ya mungu fulani aliyeonekana kama nyota

Jumanne
Jump to navigationJump to search
Jumanne ni siku ya tatu ya katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumatatu na Jumatano.
Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "4" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa ambayo ni siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "ya tatu" (ثلاثاء - thalatha).
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya tatu", kwa mfano Kiindonesia (selasa - tatu) au Kiajemi (Farsi) (سهشنب - se shanbe tatu jumamosi).
Katika lugha za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "mardi" (siku ya Mars) au Kiingereza "Tuesday" (siku ya Tiu).

Jumatano
Jump to navigationJump to search
Jumatano ni siku ya nne katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumanne na Alhamisi.
Siku ya tatu au siku ya nne?
Kuna nchi zilizobadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "5" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita أربعاء arba'a (ya nne).
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya nne", kwa mfano Kiindonesia (Rabu - ya nne) au Kiajemi (Farsi) (چهارشنبه - tchahor shanbe - siku ya nne).
Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Mercredi" (siku ya Mercurius) au Kiingereza "Wednesday" (siku ya Wodan).

Alhamisi
Jump to navigationJump to search
Alhamisi ni siku ya tano katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumatano na Ijumaa. Katika hesabu ya kimataifa ya ISO 8601 ni siku ya nne.
Wikendi katika nchi za Kiislamu
Nchi kadhaa za Waislamu huanza mapumziko ya wikendi kwenye Alhamisi kama Ijumaa ni siku ya mapumziko. Hii si nchi zote za Kiislamu. Kwa mfano Misri wafanyakazi huanza wikendi Alhamisi na kuendelea Ijumaa; Uturuki inatumia wikendi ya magharibi yaani Jumamosi-Jumapili.
Siku ya tano au siku ya nne?
Katika muundo wa juma wa kibiblia Alhamisi ni siku ya tano. Kanuni ya ISO 8601 ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hivyo Alhamisi ni namba 4. Jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea hesabu ya kale.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "5" ndani yake lakini haieleweki kirahisi kwa sababu Alhamisi ina asili ya lugha ya Kiarabu. خميس (khamis) ni namba tano tu. Kiswahili chenyewe chatumia namba hii katika jina la siku ya Jumatano inayotangulia Alhamisi. Pamoja na Ijumaa ni siku ya pekee yenye jina la Kiarabu katika lugha ya Kiswahili.
Majina ya siku zingine yameanzishwa upya katika Kiswahili kuanzia siku ya sala ya pamoja ya Waislamu kwenye Ijumaa kuzitaja kama Juma-mosi, Juma-pili n.k.
Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuita siku hiyo kwa namba "tano". Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya tano", kwa mfano Kiindonesia (Kamis - ya tano) au Kiajemi (Farsi) (پنجشنبه - panch shanbe - siku ya tano).
Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Jeudi" (siku ya Jovi au Jupiter) au Kiingereza "Thursday" (siku ya Thor).

Ijumaa
Jump to navigationJump to search
Ijumaa ni siku ya sita katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Alhamisi na Jumamosi. Katika hesabu ya kimataifa ya ISO 8601 ni siku ya tano.
Nchi kadhaa za Waislamu wengi zimeanza kutumia Ijumaa kama siku ya mapumziko kwa wafanyakazi na sehemu ya wikendi.
Siku ya tano au siku ya sita?
Katika muundo wa juma wa kibiblia Ijumaa ni siku ya sita. Kanuni ya ISO 8601 ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea hesabu ya kale.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku halina namba ndani yake. Inaitwa kufuatana na lugha ya Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu "ijumaa" kutoka neno la Kiarabu الجمعة al-juma'a yaani siku ya "jumuiya" ya Waislamu kukutana pamoja kwa sala kuu ya Ijumaa mchana. Pamoja na Alhamisi ni siku ya pekee ya juma yenye jina la Kiarabu.
Majina ya siku zingine yameanzishwa upya katika Kiswahili kuanzia Ijumaa kuzitaja kama Juma-mosi, Juma-pili n.k.
Lugha nyingi za nchi za Waislamu zafuata kawaida ileile zikitumia neno hili la Kiarabu kwa mfano kwa mfano Kiindonesia ni "Jumat" au Kitartari ambayo ni lugha ya Kiturki ni "Comğa" na kwa Kiuzbekistan ni Жұма (juma).
Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Vendredi" (siku ya Veneri /Venus) au Kiingereza "Friday" (siku ya Freya).
Katika Uislamu
Katika mfundisho ya Mtume Muhammad mojawapo ni kuitukuza siku hiyo ya Ijumaa, kwani ni siku tukufu iliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu na kupatiwa umma wa mwisho.
Mtume Muhammad alikhusisha baadhi ya vitendo katika siku ya Ijumaa:
Kusoma Surat Sijdah na Surat Insaan katika swala ya Al-Fajiri. Imepokewa na Abu Hureirah {Alikuwa Mtume akisoma katika swala ya Al-Fajri siku ya Ijumaa (Surat Sijdah) katika rakaa ya kwanza. Na katika rakaa ya pili (Surat Insaan)} Muslim.
Kusoma Surat Al-Kahfi. Amesema Mtume. {Mwenye kusoma Surat Al-Kahfi siku ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu anampa mwangaza baina ya Ijumaa mpaka Ijumaa nyingine}. Al-Bayhaqi na Haakim.
Kuzidisha kwa wingi kumsalia Mtume Muhammad. Amesema Ibnu-Qayyim: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na siku ya Ijumaa ni bwana wa siku zote. Kumswalia Mtume siku hii ina malipo mengi kushinda siku nyingine”.
Kuzidisha kumuomba Allah katika siku hii. Kwa sababu kuna wakati wa kukubaliwa dua ya Muislamu. Amesema Mtume: [Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo hali akiwa anamuomba Allah, ila Mwenyezi Mungu humkubalia Dua yake]

Jumamosi
Jump to navigationJump to search
Jumamosi ni siku ya saba katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Ijumaa na Jumapili. Katika hesabu ya kimataifa ya ISO 8601 ni siku ya sita.
Katika kawaida ya utamaduni wa magharibi Jumamosi imekuwa siku ya kuanza wikendi ikiwa ni siku ambako wafanyakazi wengi hupunzika au hufanya kazi nusu siku tu.
Katika Israeli Jumamosi huheshimiwa kama Sabato ya kibiblia. Wikendi ya Israel inaanza siku ya Ijumaa na kuendelea Jumamosi.
Siku ya saba au siku ya sita?
Katika muundo wa juma wa kibiblia Jumamosi ni siku ya saba. Kanuni ya ISO 8601 ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hivyo Jumamosi kuwa namba 6. Jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea kutumia hesabu ya kale.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "mosi" (moja) ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni wa Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi. Hesabu inaanza baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa ambayo ni siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kuwa siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinatumia jina la Kiyahudi na kuiita siku ya سبت (sabat) yaani Sabato.
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita vilevile "Sabato" kwa mfano Kiindonesia (Sabtu) au Kiajemi (Farsi) (شنبه - shanbe, kutoka "shabat").
Katika lugha kadhaa za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya mungu aliyeabudiwa zamani za dini ya Kiroma kama vile Kiholanzi "Zaterdag" au Kiingereza "Saturday" (yote: siku ya Saturnus). Lakini lugha zaidi za Ulaya hutumia pia jina la Sabato kwa namna mbalimbali kwa mfano Kifaransa "samedi" (kutoka Kilatini sambati dies - siku ya Sabato), Kihispania "Sábado", Kirusi Суббота (subbota - Sabato).

0 Reviews:
Post a Comment