TIBA
Tiba (au: Uganga) ni elimu kuhusu magonjwa ya binadamu mwilini na rohoni, jinsi ya kuzuia magonjwa na kurudisha uzima. Matibabu ni muhimu kwa afya ya binadamu na yanahitajika sana ili kumpa maisha mazuri.
Tiba imeendelea kiasi cha kuwa na matawi yanayoangalia hasa:
magonjwa ya sehemu fulani tu ya mwili, kwa mfano tiba ya moyo, ya ngozi, ya viungo vya ndani, au
aina ya tiba, kwa mfano upasuaji, au
aina ya watu, kwa mfano magonjwa ya watoto na kadhalika.
Kila somo dogo lina wataalamu wake.
Watu wanaoshughulikia magonjwa ya watu huitwa matabibu au waganga. Mara nyingi watu huwaita "daktari", lakini neno hili lamaanisha zaidi cheo cha kufaulu chuo kikuu kwenye ngazi ya juu; mara nyingi waganga husoma hadi cheo cha daktari wa tiba.
Watu wanaofanya kazi pamoja na tabibu ni muuguzi (nesi) na wasaidizi wengine.
Elimu hiyo inayofuata mbinu za kisayansi ni tofauti na uganga wa kienyeji au wa kimila.
TIBA KATIKA MAGONJWA
Ugonjwa au maradhi ni hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho inayoathiri vibaya ustawi au starehe ya kiumbehai. Hivyo hakuna tofauti kamili baina ya ugonjwa na hali ya kujisikia vibaya.
Sayansi inayochungulia magonjwa ni sayansi ya tiba.
Magonjwa yanaweza kugawanyika kutokana na vyanzo/asili zake kama vile:
magonjwa ya kuambukiza
magonjwa ya kurithi
magonjwa kutokana na ajali
magonjwa kutokana na dutu za nje ya mwili (sumu, asidi) au moto
magonjwa ya kansa
magonjwa yaliyosababishwa na tiba
magonjwa yaliyosababishwa na mfumo wa kingamaradhi uliomo mwilini
magonjwa ya nafsi
magonjwa ya roho
0 Reviews:
Post a Comment