KUNAFAIDAGANI YA MUDA KATIKA MAISHA YA VIUMBE?
1.MUDA
Muda ni sisawasawa na siku katika masiku ya siku 7
2.Msaa ni hesabu zinazo tajwa kwa kumaanisha uwepo wa naangapi katika masaa 12 yasiku na masaa ya usiku 12 ambayo ni sawa na masaa 24
Muda ni kipindi ambacho mtu aidha alifanya, anafanya au anatarajia kufanya jambo fulani. Katika maisha tumepitia vitu mbalimbali, baadhi tunaweza tukavikumbuka na vingine hatuvikumbuki, na katika maisha kadri muda unavyokwenda ndivyo vitu vinazidi kugunduliwa kutokana na ongezeko la sayansi.
Katika maisha ya kila siku mwanadamu hutegemea sana muda ili kufanikisha malengo yake.
Matumizi ya muda
Muda hutumika na watu mbalimbali kwa mambo mbalimbali kama itakavyoelezwa hapa chini:
mwanafunzi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujisomea.
mfanyakazi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.
Endapo watautumia muda huo vibaya, hakika hawataweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Hata hivyo ni muhimu kuwa na uwiano mzuri katika matumizi ya muda, kwa mfano, kwa sala na kazi.
MASAA
Saa ni kipimo cha wakati. Si kipimo cha SI kamili kama ilivyo sekunde lakini ni kawaida kote duniani pia katika matumizi ya kisayansi.
Saa inagawiwa kwa dakika 60 na sekundi 3,600. Siku ina takriban masaa 24.
Wakati ni neno la kutaja ama ufuatano wa matokeo au muda ama kipindi ambamo jambo latokea.
Tunaishi katika wakati na tunapanga maisha yetu kufuatana na wakati lakini si rahisi kusema wakati ni kitu gani. Sayansi, fizikia, falsafa na dini zote zina njia mbalimbali za kuangalia na kueleza wakati
Wakati kama mpito
Katika maarifa ya kila siku wakati ni utaratibu wa mfululizo wa matokeo. Tunaweza kuona ya kwamba jambo liliwahi kutokea (wakati uliopita), linaendelea sasa (wakati wa kisasa) na tunatarajia litaendelea katika wakati ujao. Hivyo ndivyo tunatazama maisha yetu tukikumbuka mambo yaliyopita, tunasikia hali au mambo yanayoendelea na kutegemea kuona siku inayokuja.
Kwa sababu hiyo kuna usemi kama "wakati unapita" au "wakati unakimbia".
Wakati kisayansi
Sayansi hutumia wakati kwa vipimo vingi hata kama haijui wakati mwenyewe ni kitu gani. Imeunda vipimo vya wakati mwenyewe vinavyowezesha kuelewa matokeo na kuyalinganisha.
Hapa sayansi inajaribu kuona wakati kama wanda (dimensioni) moja ya ulimwengu pamoja na zile tatu za nafasi ya ulimwengu. Hapa huitwa "wanda ya nne" (the fourth dimension).
Tofauti yake na nyanda za nafasi ni ya kwamba wakati una mwendo na mwelekeo.
Vipimo vya kawaida vya wakati
Vipimo vya wakati hutumia matokeo yanayorudia mara kwa mara bila mabadiliko.
Kipimo cha kawaida ni siku au kwa lugha nyingine muda wa mzunguko 1 wa dunia yetu unaonekana kwetu kutokana mabadiliko ya mchana na usiku.
Muda huu wa Mzunguko mmoja hugawiwa kwa masaa 24 na kuitwa "siku". Saa hugawiwa kwa dakika 60 na kila dakika kwa sekunde 60.
Mbio mmoja wa dunia yetu kuzunguka jua huitwa "mwaka". Utaratibu wa miaka hupangwa kwa njia ya kalenda.
Vipindi kama mwezi na wiki hupanga siku ndani ya kalenda.
Vipimo vya Kisayansi
Sayansi haijaridhika tena na vipimo hivi vya kawaida. Mizunguko ya dunia au siku hazilingani kikamilifu. Hapa sayansi imeondoka katika siku kama msingi wa vipimo vya wakati. Badala yake imechukua muda wa sekunde na kukiliganisha kwa mwendo wa atomi.
Katika vipimo sanifu vya kimataifa sekunde imewekwa kama muda wa radidi (periodi) 9,192,631,770 za mnururisho wa atomi ya caesi ya 133Cs.
Kisayansi Saa dio chombo maalum hutumka kupima wakati hasa saa za kronogilafia (chronograph watches) - saa zijulikanazo kwa Kingereza kama "Stop-Watch" za kupimia mda mfupi wakati tukio kama shindano la riadha zinafanyika
Vipindi vya wakati
milenia = miaka 1000
karne = miaka 100
mwaka = miezi 12 = siku 365.25
mwezi ≈ wiki 4 ≈ siku 30
wiki (juma)= siku 7
siku = masaa 24
saa = dakika 60
dakika = 60 sekunde
sekunde = 1000 millisekunde
milisekunde = 1000 mikrosekunde
mikrosekunde = 1000 nanosekunde
nanosekunde= 1000 pikosekunde
pikosekunde= 1/1,000,000,000,000 sekunde
1.MWAKA 2028
Mwaka ni kipindi cha takriban siku 365 katika Kalenda ya Gregori ambayo imekuwa kalenda ya kawaida kimataifa ikifuata mwendo wa jua.
Mwaka katika kalenda ya jua
Katika kalenda za jua mwaka unalingana na muda wa mzunguko mmoja wa dunia kwenye mzingo wake kuzunguka jua letu.
Muda kamili wa mzunguko huu ni siku 365.2425.
Kwa sababu hiyo kalenda ya Gregori inaongeza mwaka mrefu wa siku 366 katika utaratibu ufuatao:
kila mwaka wa nne utakuwa na siku 366 badala ya 365 kwa kuongeza tarehe 29 Februari. Mifano: 1892, 1996, 2004, 2008, 2012
kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 100 utakuwa na siku 365 (siyo 366 hata kama namba za miaka hii zinagawiwa kwa 4 pia!). Mifano: 1700, 1800, 1900, 2100
kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 400 utakuwa tena na siku 366 (siyo 365 hata kama namba za miaka hii zinagawiwa kwa 100 pia!). Mifano: 1600, 2000, 2400, 2800
Miaka katika kalenda mbalimbali
Katika kalenda mbalimbali kuna mahesabu tofauti ya muda wa mwaka.
Mwaka wa Kiislamu ni mwaka wa mwezi una siku 354.
Mwaka wa Kiyahudi unafuata pia kalenda ya mwezi lakini kwa namna ya pekee ya kuupatanisha na mwendo wa jua; muda wake ni siku 354 lakini kila baada ya miaka miwili au mitatu kuna mwaka mrefu kwa kuongeza mwezi mmoja. Kwa jumla mwezi huingizwa mara 7 katika kipindi cha miaka 19.
Kalenda za kihistoria ya Wamaya katika Amerika ya Kati ilikuwa na aina ya mwaka mwenye kipindi cha siku 260 iliyounganishwa na mwaka wa jua wa siku 365 katika utaratibu wa miaka 52.
Kalenda ya mwaka wa Kanisa ni kalenda inayoratibu sikuu za kikristo na utaratibu wa liturgia kama vile masomo ya Biblia kwa ajili ibada mbalimbali. Hii ni lazima kwa sababu namna ya kuratibu mwaka si miezi bali wiki na jumapili. Kalenda hii hutofautiana kiasi kati ya makanisa yenye mapokeo ya kiorthodoksi upande mmoja na kanisa katoliki upande mwingine. Waorthodoksi huhesabu kwenye msingi wa kalenda ya Juliasi na Wakatoliki huhesabu kwenye msingi wa kalenda ya Gregori. Makanisa ya kiprotestant kama vile Anglikana na Walutheri hufúata mapokeo ya kikatoliki. Tofauti si muda wa mwaka lakini mwanzo wake. Mwaka wa Kanisa huanza kewenye jumapili ya kwanza ya majilio au Adventi
2.MWEZI NA TAREHE
Mwezi ni mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka. Muda wa mwezi unategemea aina ya kalenda inayotumika
Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara 1 ni siku 29 1/4.
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu.
Inawezekana kwamba juma la siku saba lilianza kwa kuzingatia robo 4 za mwezi wa siku 28.
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ndiyo kalenda ya Kiislamu inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.
1,Januari , siku 31
2,Februari , siku 28
3,Machi , siku 31
4,Aprili , siku 30
5,Mei , siku 31
6,Juni , siku 30
7,Julai , siku 31,
8,Agosti , siku 31
9,Septemba , siku 30
10,Oktoba , siku 31
11,Novemba , siku 30
12,Desemba , siku 31
kwa kiarabu
Muharram محرّم
Safar صفر
Rabi`-ul-Awwal (Rabi' I) ربيع الأول
Rabi`-ul-Akhir (Rabi' II) ربيع الآخر أو ربيع الثاني
Jumaada-ul-Awwal (Jumaada I) جمادى الأول
Jumaada-ul-Akhir (Jumaada II) (Jumaada II) جمادى الآخر أو جمادى الثاني
Rajab رجب
Shaaaban شعبان
Ramadan رمضان
Shawwal شوّال
Dhul Qaadah ذو القعدة
Dhul Hijjah ذو الحج
4.SIKU KATIKA SIKU 7 YANI
Juma (kutoka neno la Kiarabu) au wiki (kutoka Kiingereza "week") ni kipindi cha siku saba. Kila siku ina jina lake.
Katika mwaka wa kalenda ya Gregori mna majuma 52 pamoja na siku moja au mbili za ziada. Hesabu ya majuma inaendelea mfululizo bila ya kuanza upya wakati wa mwaka mpya.
Ufuatano wa majuma haulingani na mgawanyo mwingine wa wakati kwa njia ya miezi au mwaka.
Mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo
Asili ya juma ni katika utamaduni wa kale wa Mashariki ya Kati tangu Babiloni. Imeenea duniani kote kupitia Biblia na desturi za Uyahudi na Ukristo.
Ufuatano wa siku katika mapokeo hayo huanza na Jumapili. Majina ya siku ni kama yafuatayo:
Jumapili (Dominika)
Jumatatu
Jumanne
Jumatano
Alhamisi
Ijumaa
Jumamosi (Sabato)
Katika mwaka juma moja la Machi mwishoni au la Aprili linaadhimishwa na Wakristo wengi kama Juma kuu, ambapo wanaadhimisha matukio makuu ya imani yao kadiri ya historia ya wokovu, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.
Siku za Jumamosi na Jumapili mara nyingi huitwa "wikendi" (kutoka Kiingereza: "weekend", yaani mwisho wa juma). Hata hivyo katika mapokeo hayo Jumapili ni mwanzo wa wiki mpya, si mwisho wake.
Majina ya siku kwa Kiswahili
Majina ya siku tano kwa Kiswahili ni ya namba zinazoanza kuhesabiwa baada ya siku ya Ijumaa (ambayo ni siku ya sala kuu katika Uislamu): Ijumaa - Jumamosi - Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano.
Alhamisi na Ijumaa ni majina ya lugha ya Kiarabu inayofuata mapokeo ya Kiyahudi kuhusu majina ya siku.
Hivyo "Alhamisi" ina maana ya "siku ya tano" (baada ya Jumamosi inayoitwa "sabat" kwa Kiarabu, sawa kama "shabbat" kwa Kiebrania (lugha ya Wayahudi).
"Ijumaa" ni matamshi ya Kiswahili ya jina la Kiarabu la "jum'a" inayomaanisha "siku ya mkutano" (= ya kusali pamoja)
ILI KUJUWA FAIDA ZA MASAA NA MAANA YAKE
unapaswa kujuwa kila saa ina kuwa na maana yake katika kila jambo utakalo taka kulifanya hapa kwenye linki hii utajuwa masaa pamoja na kila kinacho husika katika saa ikiwa unahitaji kufanya chochote katika shugulizako unatakiwa kupanga muda nakujifunza kufanya mambo yako kwamuda
bonyeza hapa kupata 👉{YANAYO HUSU KILA SAA KATIKA MASAA 12}👈
0 Reviews:
Post a Comment